Mkuu wa Mkoa Tanga akabidhi msada kwa wahanga wa mafuriko
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigela amekabidhi msada kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea mwishoni mwa mwaka. Msada huo ulitolewa na kampuni ya Cocacola Kwanza ya Dar es salaam kwa ajili ya Halmashauri tatu za wilaya ambazo ni Korogwe, Lushoto na Handeni. Makabidhiano hayo ya msada yalifanyika Januari 29, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Wakati wa makabidhiano Mh. Shigela aliishukuru kampuni ya Cocacola Kwanza kwa msada waliotoa kwa wananchi waliopata maafa. Mwishoni mwa mwaka jana mvua zilinyeesha na kusababisha madhara makubwa kwa wananchi ikiwemo uharibifu wa makazi na mali mbalimbali. Msada uliyotolewa na kampuni ya Cocacola Kwanza ni pamoja na Magodoro mia tatu (300), Shuka mia tatu (300), Vyandarua mia moja na hamsini (150), Maharage kilo mia mbili na arobaini (240), Mchele kilo mia tano (500) na Mafuta ya kupikia lita mia tano (500).
Katika makabidhiano hayo Wakuu wa Wilaya pia walishiriki akiwemo Mh. Kissa Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mh. January Lugangika Mkuu wa Wilaya ya Lushoto pamoja na Mh.Boniface Maiga ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni. Waheshimiwa wote waliishukuru kampuni ya Cocacola Kwanza kwa msada waliotoa kwani wameonesha utu, umoja na mshikamano kwa wahanga wa mafuriko.
Nae Bwana Victor Byemelwa ambaye ni Afisa Mawasiliano wa kampuni ya Cocacola Kwanza alisema kuwa msada waliotoa ni jitihada za kampuni kutoa pole kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea mwishoni mwa mwka jana. Kwa upande mwingine Ndugu Faraji Abdallah na Bi. Zaina Ramadhani ambao ni waathirika wa mafuriko waliishukuru kampuni ya Cocacola Kwanza na Serikali kwa ujumla kwa kuwapatia msada.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.