UTARATIBU WA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI
Kibali cha Ujenzi ni kibali kinachotolewa na Halmashauri chini ya Sheria ndogo za Udhibiti wa ujenzi holela mijini na ambacho kitamruhusu mwananchi afanye ujenzi au ukarabati wa jengo.
UMUHIMU WA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
•Kutimiza takwa la sheria ndogo za jiji
•Kuwezesha kujenga majengo na nyumba kama yalivyoelekezwa katika mipango miji wa jiji
•Kudhibiti ujengo holela
TARATIBU & KANUNI ZA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI
Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri. Report submitted for Approval (RPA)”. Fomu hii imegawanyika katika sehemu tano (5), zinazohusisha wataalamu wafuatao;
•Mkaguzi wa Majengo (Building Inspector)
•Afisa Ardhi (Land Officer)
•Mpima (Land Surveyor)
•Afisa Mipango Miji (Town Planning Officer)
•Afisa Afya (Health and Sanitation Officer)
Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri Fomu itaambatanishwa na michoro iliyokamilika yaani “Architectural & Structural Drawings” na kupita kwa wataalamu wote watano (5) kama ilivyoonyeshwa hapo juu kwa ajili ya uhakiki kama ifuatavyo.
i.Mkaguzi wa Majengo (Building Inspector) - kuona kama michoro inakidhi haja ya kiufundi na specifications.
ii.Afisa Ardhi (Land Officer) – kuona kama umiliki wa eneo linaloendeleza ni halali, kukagua hati miliki, nk.
iii.Mpima wa Jiji (Land Surveyor) – kutambua mipaka halali
iv.Afisa Mipango Miji wa Jiji (Town Planning Officer) – Kuona kama ujenzi unaoombewa ni sahihi kwa mujibu wa michoro ya mipango miji, eneo la maegesho lipo, nk
v.Afisa Afya (Health and Sanitation Officer) – kuona kama usafi kwa ujumla na maji taka yatatunzwa vyema
Kama michoro na nyaraka za umiliki zimekidhi vigezo zitawasilishwa kwenye kamati ndogo ya mipango miji na utoaji vibali
Baada ya michoro na nyaraka kupita katika kamati ndogo ya mipango miji na utoaji vibali itapigiwa makadirio na mwombaji atapaswa kulipia gharama husika kwenye akaunti ya Halmashauri atakayopewa.
Mwombaji kuandaliwa kibali cha ujenzi kinachosainiwa na mhandisi wa ujenzi na afisa mipango miji
MUDA WA UPATIKANAJI WA KIBALI CHA UJENZI
•Endapo mwombaji atakamilisha hatua zote muhimu kwa wakati atapata kibali cha ujenzi ndani ya majuma mawili (2) hadi manne (4)
•Hii ni pamoja na kuwasilishaji wa ramani zilizoidhinishwa na wataalamu husika na hati za umiliki zilizo sahihi.
WAJIBU WA MWANANCHI
•Ni wajibu wa kila mwananchi kujenga au kukarabati nyumba yake iliyo ndani ya jiji kwa kibali kutoka Halmashauri
•Wakazi wote wa katikati ya mji wanapaswa kukarabati au kujenga nyumba za kwenda juu (maghorofa) tu.
•Hairuhusiwi kujenga au kukarabati nyumba za chini.
TAHADHARI
•Endapo mwananchi yoyote atajenga au kukarabati nyumba bila kibali cha ujenzi toka Halmashauri, atapewa ilani ya kusimamisha ujenzi au ukarabati na kushauriwa kufuata taratibu za kuomba kibali cha ujenzi ndani ya siku saba (7)
•Kama mwombaji atakaidi ilani ya kusimamisha, jiji litampa ilani ya kubomoa jengo lake mwenyewe na akishindwa jiji litabomoa kjengo husika na kudai mmiliki gharama za utekelezaji wa ubomoaji huo
•Wananchi wote wa Mji wa Korogwe wanashauriwa kuacha ujenzi holela kwa kufuata sheria ndogo za ujenzi na kupata kibali cha ujenzi
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.