Jimbo la Korogwe mjini laanza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika jimbo la Korogwe Mjini limeanza rasmi leo Februari 13, 2025 na linatarajiwa kukamilika Februari 19, 2025. Zoezi hilo linatekelezwa katika vituo 80 vilivyopo katika Kata zote Kumi na Moja zinazounda Jimbo la Korogwe Mjini. Katika kipindi chote cha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, vituo vitafunguliwa Saa 2: 00 Asubuhi na vitafungwa Saa 12: 00 Jioni.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.