Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope anawakaribisha Wananchi wote wa Korogwe Mji kwenye maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kanda ya Mashariki yanayofanyika Halmashauri ya manispaa ya Morogoro 2025 kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. Kwa upande mwingine Bi. Mwashabani Mrope alipata wasaa wa kutembelea banda la Halmashauri ya Mji wa Korogwe kujionea Shughuli zinazofanywa.
Katika matembezi hayo Mkurugenzi alijionea Shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Korogwe katika maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Manispaa ya Morogoro. Maonesho ya Nanenane ya Mwaka huu yanafanyika kuanzia Agosti 1 mpaka yatakapohitimishwa Agosti 8,2025. Kauli mbiu ya Mwaka huu inasema “Chagua Viongozi Bora kwa maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.