Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe atembelea ujenzi wa miradi ya maendeleo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope akiambatana pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo ametembelea ujenzi wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu ili kujionea utekelezaji wa miradi hiyo. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa sekondari mpya Kata ya Majengo, ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Kwakombo, Kilole. Matondoro, pamoja na Mtonga. Mradi mwengine ni ujenzi wa bweni shule ya sekondari Ngombezi pamoja na ujenzi wa nyumba ya Walimu shule ya sekondari Msambiazi. Ziara hiyo ilifanyika Desemba 19, 2024 katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.