• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Mji wa Korogwe
Halmashauri ya Mji wa Korogwe

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Korogwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Ardhi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi waJamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
    • Mifugo
    • Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Za afya
    • Kielimu
    • Za Maji
    • Za kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Elimu, afya,uchumi na maji
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Picha za Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Mkoa wa Tanga atembelea ujenzi wa Vituo vya afya Korogwe

Posted on: November 15th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Tanga  atembelea ujenzi wa Vituo vya  afya Korogwe

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima akiambatana pamoja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kalist Lazaro Bukhay ametembelea miradi ya ujenzi wa Vituo vya Afya katika Wilaya ya Korogwe. Miradi hiyo ya ujenzi wa Vituo vya Afya inajumuisha Kituo cha Afya cha Mgombezi na Kituo cha Afya cha Kwamsisi vilivyopo Halmashauri ya Mji wa Korogwe pamoja na Kituo cha Afya cha Mnyuzi kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe. Ziara hiyo ya kutembelea miradi ya ujenzi wa Vituo vya Afya  imefanyika Novemba 15, mwaka huu.

Kupita fedha za makato ya tozo ya miamala ya simu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipatia Wilaya ya Korogwe kiasi cha Shilingi Milioni 750 za awali kwaajili ya utekelezaji wa ujenzi wa Vituo  vitatu  vya Afya ambavyo ni Mgombezi, Kwamsisi pamoja na Mnyuzi ikiwa kila kituo kimepatiwa kiasi cha Shilingi Milioni 250.

Baada ya utekelezaji wa ujenzi wa majengo ya awali katika Kituo cha  afya Mgombezi, Kwamsisi pamoja na Mnyuzi kukamilika, Serikali itaongeza fedha nyingine kiasi cha Shilingi Milioni 750 ili kukamilisha ujenzi wote wa vituo vyote vitatu katika Wilaya ya Korogwe  ikiwa kila kila Kituo cha Afya  ujenzi wake utagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 500.

“Muwe na uchungu na mradi huu kama mali za familia zenu” alisema Mhe. Adam Malima ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga wakati wa ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa  Vituo vya Afya katika Wilaya ya Korogwe. Mhe. Malima alisisitiza kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Korogwe wakamilishe miradi hiyo ya vituo vya afya kwa wakati  ili iweze kuwahudumia Wananchi.

Katika hatua nyingine Mhe. Malima amemuagiza Kaimu Mkuu wa Wilaya Korogwe Mhe. Kalist Lazaro Bukhay pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili za Wilaya hiyo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa Vituo vyote vya afya ifikapo Januari 2022. Mhe Malima alisisitiza kuwa fedha zote za miradi zimeshaingizwa katika Halmashauri hivyo hakuna sababu ya msingi itakayosababisha uhaba wa vifaa vya ujenzi kwajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

 “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa maelekezo yote uliyotoa tumeyapokea na tutayafanyia kazi” alisema Mhe. Kalist Lazaro Bukhay ambaye ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe wakati wa  ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa Vituo vya Afya. Mhe. Bukhay alifafanua kuwa yeye pamoja na viongozi kutoka Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Korogwe watahakikisha wanafanya kazi kwa bidi ili itakapofikia Januari 2022 ujenzi wa vituo vyote vitatu vya afya uwe umekamilika.

Kwaupande mwengine, Wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe  pamoja na  Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ambao ni wanufaika wa miradi ya ujenzi wa Vituo cha Afya  walitoa shukrani  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha  kwaajili ya  ujenzi wa Vituo vya Afya.

Matangazo

  • Tangazo la Kazi - Afya December 06, 2024
  • TANGAZO LA KAZI - AFYA November 26, 2024
  • ERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN KOROGWE TOWN UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Waratibu Elimu kata na Wali Wakuu wa Shule za Msingi za Mji wa Korogwe wajengewa uwezo wa usimamizi wa ufundishaji na Ujifunzaji.

    June 27, 2025
  • Mradi wa TACTIC kuimarisha Huduma za Usafirishaji kwa Miji 12 Tanzania.

    June 26, 2025
  • Halmashauri ya Mji wa Korogwe yaadhimisha Siku ya Wajane Duniani.

    June 23, 2025
  • Shule ya Msingi Kwamngumi yalima Hekari mbili za Mahindi

    June 19, 2025
  • Angalia Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa Muhimu

  • Ukodishaji wa Ukumbi
  • Ukasanyaji wa Taka

Tovuti Zinazohusiana

  • TOVUTI YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • MKOA TANGA
  • TUME YA AJIRA
  • PPRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Korogwe Tanga Tanzania

    S.L.P: 615 Korogwe

    Simu: 0272650050

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.