• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Mji wa Korogwe
Halmashauri ya Mji wa Korogwe

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Korogwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Ardhi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi waJamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
    • Mifugo
    • Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Za afya
    • Kielimu
    • Za Maji
    • Za kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Elimu, afya,uchumi na maji
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Picha za Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe azindua Kambi ya Matibabu ya Macho

Posted on: June 2nd, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe azindua Kambi ya Matibabu ya Macho

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Jokate Mwegelo amezindua Kambi ya Matibabu ya Macho katika Hospitali ya Mji wa Korogwe (Magunga). Kambi hiyo ya Matibabu ya Macho ilizinduliwa Juni 02, Mwaka  huu. Pamoja na uzinduzi wa Kambi hiyo, Kambi  tayari ilishaanza  kutoa huduma kuanzia Juni 01 na itaendelea hadi Juni 04 Mwaka huu bila ya gharama yoyote (Bure). Huduma zote za Matibabu ya Macho zinaratibiwa na Taasisi ya Al Ataa Charitable Foundation kwa udhamini wa Taasisi ya Qatar Charity.

“ Tuzingatie ushauri tutakaopewa na Wataalamu wa Macho ili tuweze  kuiamarisha Macho yetu” alisema Mhe. Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Matibabu ya Macho. Mhe. Jokate alisisitiza kuwa pamoja na Wananchi kupatiwa Matibabu ya Macho, ni vyema kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kujua hali zao na kuweza kulijenga Taifa bila hofu yoyote.

“Tunatoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupa ruhusa ya kuendelea kutao huduma za Matibabu kwa Watanzania katika kipindi chake cha uongozi” alisema Bw.  Abubakar Mwinyimbegu ambaye ni Meneja Uhusiano wa Umma kutoka Taasisi ya Al Ataa Charitable Foundation. Bw. Abubakar alifafanua kuwa Taasisi hiyo itaendelea kushikamana na Watanzania katika kutoa huduma za Matibabu.

Katika hatua nyengine, Bw. Vendavenda Sumuni ambaye ni Katibu wa Afya Katika  Halmashauri ya Mji wa Korogwe  alisema “ Huduma zote ni bure ni vyema Wananchi wakajitokeza kwa wingi katika kuchangamkia fursa ya  matibabu”. Nao Wananchi waliojitokeza kupatiwa huduma ya Matibabu ya Macho walitoa Shukrani kwa Taasisi inayoratibu Matibabu na Serikali kwa ujumla kwa kuapatiwa huduma bila gharama yoyote (Bure).

Matangazo

  • Tangazo la Kazi - Afya December 06, 2024
  • TANGAZO LA KAZI - AFYA November 26, 2024
  • ERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN KOROGWE TOWN UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Waratibu Elimu kata na Wali Wakuu wa Shule za Msingi za Mji wa Korogwe wajengewa uwezo wa usimamizi wa ufundishaji na Ujifunzaji.

    June 27, 2025
  • Mradi wa TACTIC kuimarisha Huduma za Usafirishaji kwa Miji 12 Tanzania.

    June 26, 2025
  • Halmashauri ya Mji wa Korogwe yaadhimisha Siku ya Wajane Duniani.

    June 23, 2025
  • Shule ya Msingi Kwamngumi yalima Hekari mbili za Mahindi

    June 19, 2025
  • Angalia Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa Muhimu

  • Ukodishaji wa Ukumbi
  • Ukasanyaji wa Taka

Tovuti Zinazohusiana

  • TOVUTI YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • MKOA TANGA
  • TUME YA AJIRA
  • PPRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Korogwe Tanga Tanzania

    S.L.P: 615 Korogwe

    Simu: 0272650050

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.