Mapema Februari 2, 2025 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi amekabidhi pikpiki moja kwa Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Victoria Nchimbi.
Pikipiki hiyo iliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa Mji ina lengo la kurahisisha utendaji kazi wa Idara hiyo ikiwa ni pamoja na kusaidia utambuzi wa mifugo, kurahisisha utoaji chanjo kwa mifugi ili kupunguza magonjwa ya mifugo. Bi. Zahara amemtaka Afisa huyo kutumia pikipiki hiyo katika kuongeza ufanisi katika kazi na kuhakikisha mifugo ya Korogwe Mji inatambulika na kuuzika kimataifa.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuleta pikipiki hiyo na kuahidi kuwapa tabasamu Wafugaji wa Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.