Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Korogwe Idara ina wajubu wakusimamia na kutekeleza hali ya upatikanaji wa maji katika Mji wa Korogwe kwa kuanzisha miradi mipya na kuboresha iliyopo.
Kuwezesha na kufanya matengenezo madogo madogo ya miundo mbinu ya maji kila tatizo linapotokea na kufuatana na mpango kazi wa matengenezo wa Idara.
Kutoa Elimu katika jamii zilizokwisha jengewa miradi ya maji ya visima, mambomba na uvunaji wa maji ya mvua ili miradi iweze kutunzwa na uzingatiaji wa usafi kwa afya zao.
Kusimamia na kutekeleza shughuli zote za maendeleo ya sekta ya maji katika Mji wa Korogwe na kuzitolea taarifa kila robo ya mwaka na kila zinapohitajika..