Baraza jipya la madiwani Halmashauri ya Mji Korogwe limeapishwa na kuanza rasmi majukumu yake 03/12/2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe. Katika baraza hilo Mkurugenzi Bi. Zahara Msangi amewasilisha taarifa ya utekelezaji kwa kipindi Cha July - October 2025.
Baada ya uapisho kulifanyika uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, ambapo Mheshimiwa Ally Saddiq Mkwavingwa alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri, huku Nassoro Mohamed Hassan akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Mwenyekiti mpya Ally Saddiq Mkwavingwa aliwaomba Madiwani na wataalamu wa Halmashauri kushirikiana kwa karibu katika mipango ya maendeleo ili kufanikisha malengo waliyojiwekea. Aidha, aliipongeza Ofisi ya Mkurugenzi na timu ya wataalamu kwa kusimamia vyema miradi ya maendeleo pamoja na kuibua vyanzo vipya vya mapato vitakavyoongeza uwezo wa Halmashauri kifedha.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.