Halmashauri ya Mji wa Korogwe ni moja ya Halmashauri kumi na moja katika mkoa wa Tanga na iliundwa mwaka 2005 baada ya kukua kwa Mamlaka ya Mji iliyokuwepo tangu 1996-1997. Halmashauri ya Mji wa Korogwe inapatikana katika sehemu ya kati ya Mkoa na kuzungukwa na maeneo mengine ya Wilaya ya Korogwe (ikizungukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe) ila kwa Wilaya ya Handeni upande wa kusini. Iko katika latitudo 50 na 5014’ S na katika longitudo 38023' na 30033' E.
Halmashauri ya Mji wa Korogwe ni Mji wa pili kwa ukubwa katika Mkoa wa Tanga baada ya Jiji la Tanga. Halmashauri ya Mji wa Korogwe ina kata 11 na mitaa 24 ndani ya eneo lenye Kilomita za mraba 212, ndilo eneo ndogo kuliko yote kati ya Halmashauri 11 katika mkoa wa Tanga.
Pamoja na kuwa katikati ya Mkoa, Halmashauri ya Mji wa Korogwe imeunganishwa na maeneo yote ya Mkoa wa Tanga, Mikoa ya kaskazini ya Kilimanjaro na Arusha na Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kwa upande wa kusini. Jiji la Tanga lipo umbali wa kilomita zipatazo 93 kutoka Mji wa Korogwe, Arusha kilomita ni 344 na Dar es Salaam kilomita ni 305. Halmashauri Mji wa Korogwe pamoja na Halmashauri inayoizunguka, zimekuwa kiungo muhimu kihistoria kwa wazawa na wageni kutoka nje kama vile Mashariki ya Kati na Wapelelezi wa kikoloni, wafanyabiashara, wamishenari na watawala wa kikoloni. Kwa sasa Mji wa Korogwe umekuwa kitovu cha biashara na huduma katika njia kuu za reli na barabara kutoka Dar es Salaam, Tanga na Arusha.
Mji wa Korogwe pia hutumika kama makao makuu ya utawala wa Halmashauri zote mbili. Uchumi, shughuli za kijamii, miundombinu na utawala katika Halmashauri zote mbili vinategemeana na ni jumuishi.
HALMASHAURI YA MJI WA KOROGWE
MPANGILIO WA KIKANDA
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.