Kuratibu maandalizi ya bajeti ya maendeleo kila mwaka kwa njia ya mipango shirikishi
Kukusanya mipango ya maendeleo kutoka kata na idara mbalimbali na kuandaa Mpango wa maendeleo wa Halmashauri.
Kutoa taarifa ya kiwango cha chini (kata na mtaa) ambayo miradi kupitishwa kwa ajili ya mwaka wa fedha kwa kila kata na kiasi cha fedha kilichopitishwa.
Kuandaa Mpango Kazi na mtiririko wa fedha kwa bajeti iliyopitishwa na kutuma kwa Katibu Tawala Mkoa kwa ajili ya uingizaji wa fedha na utekelezaji wa miradi.
Kuratibu maandalizi ya taarifa ya kifedha ya kila robo na utekelezaji wake ambayo itaonyesha utoaji/utumiaji wa fedha kwa robo nyingine.
Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kufuatiliaji takwimu mbalimbali na kuhifadhi ili kuziwezesha Idara nyingine katika maandalizi ya taarifa mbalimbali na makadirio ya bajeti. i