Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema aongoza zoezi la usafi wa kufungua Mwaka 2026, zoezi hilo limefanyika Januari 3, 2026 katika Kata ya Kwamkole barabara inayoelekea nyumbani Kwakmkole ikiwa ni ishara ya kuwaonya wanaotupa taka katika eneo hilo kuacha mara moja.
Mhe. Mwakilema amekemea vikali vitendo vya Wananchi wanaowatuma bodaboda na bajaji kutupa takataka katika eneo hilo kwani linasababisha uchafu wa eneo na kuharibu chanzo cha maji ya mto Mbeza. Pia amemuelekeza Afisa Mazingira kuweka doria maalum ili kuwabaini na kuhakikisha tabia hiyo hairudii tena.
Aidha amewashukuru Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kuhudhuria na kuandaa zoezi hilo na kuwaomba liwe endelevu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.