
Wananfunzi wenye umri wa miaka 5 mpaka miaka 14, wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wamepatiwa dawa za kinga tiba dhidi ya minyoo tumbo, dawa zilizotolewa kwa shule zote za msingi katika halmashauri hiyo limefanyika Februari 12, 2026 ambapo na kutekelezwa chini ya usimamizi wa Mratibu wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele akishirikiana na walimu kwa kila shule husika.

Dawa hizo zinatolewa kwa watoto wa umri huo,
ikiwa ni mpango wa kitaifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, kwa watoto wote wa umri huo.

Afisa wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Veronica Mjema akiwa katika ziara ya kuzitembelea shule zilizopo Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa ajili ya kuangalia mwenendo mzima wa zoezi la ugawaji dawa za minyoo ya kichocho na minyoo ya tumbo kwa wanafunzi wa Shule za Msingi 40 alisema kuwa ameridhika na maandalizi ya watoto shuleni kwani kila shule imewandaa watoto vizuri kwa kuwa elimisha umuhimu wa kumeza dawa za minyoo ya tumbo na kichocho.
Mjema aliongeza kuwa utekelezaji wa zoezi hilo unaendelea vizuri kwani kila shule imeandaa mazingira safi ya kugawia dawa na pia walimu wamehakikisha kila mtoto ana pata chakula cha kutosha kabla ya kunywa dawa hizo.
Aliwasisitiza Walimu hao kuendelea kuwa karibu na wanafunzi hao pamoja na kuwapatia elimu ya kuwaondoa hofu baada ya kunywa dawa hizo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.