Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu katika mfumo rasmi na Elimu nje ya mfumo rasmi katika Halmashauri..
Kuandikisha watoto wa darasa la kwanza wenye umri wa miaka wa kwenda shule.
Kuelimisha jamii kushiriki katika mambo mbali mbali ya shule kupitia vikao vya mitaa ambavyo wananchi watahudhuria na kutoa maoni.
Kuandaa bajeti ya idara na vitengo vyake ikiwa ni pamoja na mpango kazi unaoendana na bajeti hiyo.
Kusimamia na kuendeleza taaluma katika Mji wa Korogwe kwa kusimamia ufundishaji, mahudhurio ya walimu na wanafunzi na utendaji kazi kwa ujumla.
Kuandaa takwimu mbalimbali za kielimu za wanafunzi, walimu, samani na miundombinu.
Kuratibu mashindano ya taaluma na michezo kwa shule za msingi.
Kusimamia haki na maslahi ya walimu kwa kufuata taratibu kama vile posho,ruhusa, likizo,masomo,matibabu n.k.
Kuhudumia jamii kuhusiana na mambo yote ya kielimu na mafunzo mbalimbali kupitia kamati za shule na shuguli nyinginezo kama vile uhamisho wa wanafunzi.
Kuandaa na kuendesha vikao mbalimbali vya wadau wa elimu katika ngazi zote za Halmashauri.
Kuandaa Tange ya walimu wa shule za msingi kwa kila mwaka.