1.0 UTANGULIZI:
Idara ya Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana ni kati ya idara za Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Idara ina vitengo vya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana,ambapo majukumu yake ni kuratibu na kusimamia upatikanaji wa huduma za jamii na utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika ngazi ya jamii. Katika utekelezaji wake Idara inaratibu mipango ya maendeleo ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF - Tanzania Social Action Fund), Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (CHF– Re-organized Community Health Fund), Mpango wa Kudhibiti UKIMWI, Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) na Kuratibu asasi zisizokuwa za ki serikali (NGOs & CBOs) na vikundi vya kiuchumi.
2.0 Muundo na Rasilimali watu.
Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana katika Halmashauri ya Mji Korogwe ina vitengo vitatu, ambavyo ni kitengo cha Maendeleo ya Jamii, kitengo cha Ustawi wa Jamii na Kitengo cha Vijana.Watumishi wa idara hii ni Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa jamii, na Afisa Vijana.
3.0 Majukumu yanayotekelezwa na idara
Idara kwa kutumia rasilimali mbalimbali zilizopo utekeleza majukumu yake kwa mgawanyo unaozingatia taaluma na miundo ya serikali.
3.1 Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
3.2 Kitengo cha Ustawi wa Jamii
3.3 Kitengo cha Vijana
Lengo kuu la Kitengo;
Kusaidia vijana kupata mbinu za kujiinua kiuchumi na kutambua fursa na vikwazo vilivyo katika mazingira yao na kujiletea maendeleo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.