FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE .
1.1 UTANGULIZI.
Halmashauri ya Mji wa Korogwe ipo katikati ya Mkoa wa Tanga kaskazini mashariki mwa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe. Mji wa wa Korogwe ni wa pili kwa ukubwa katika Mkoa wa Tanga ikifuatiwa na jiji la Tanga. Halmashauri ya Mji wa Korogwe ina Kata 11, Mitaa 22 na vijiji 7 ikiwa na eneo la mita za mraba 212. Mji wa Korogwe una wakazi wapatao 68,308 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012. Milima ya usambara inayozunguka Mji wa Korogwe na mito inayotiririsha maji pamoja na mto pangani unawezesha Mji wa Korogwe kuwa mahali pazuri kwa ajili ya kuishi , kuwepo kwa shughuli za viwanda,kilimo , utalii na huduma za jamii .
1.2 HALI YA HEWA.
Halmashauri ya Mji wa Korogwe ina hali nzuri ya hewa ikiwemo misimu miwili ya mvua Masika ina kipindi kirefu kuanzia mwezi Februari hadi mwezi Mei na kipindi kifupi cha vuli kinachoanzia mwezi Septemba hadi Novemba. Wastani wa mvua kwa mwaka ni mililita 950 (900-1000), Mwezi Novemba hadi machi ni kipindi cha joto kali kiasi cha nyuzi joto(30 – 32 ) kwa nyakati za mchana kipindi cha baridi kinaanza mwezi Mei hadi Oktoba kikiwa na kiasi cha nyuzi joto (23 – 25). Upande wa kaskazini wa Mji kuna ukanda wa juu wa milima wa wastani wa mita 1200 kutoka usawa wa bahari ikizungukwa na misitu ya asili inayovutia shughuli za utalii kufanyika hapa.
2.0 FURSA ZILIZOPO.
Fursa zilizopo ni za uwekezaji katika maeneo yafuatayo :-
NA |
SEKTA |
ENEO LA UWEKEZAJI(MAHALI NA UKUBWA) |
HALI/HATUA ILIYIFIKIWA |
MAONI/MAELEZO |
|
1.
|
USAFIRISHAJI
Bandari kavu kwa usafirishaji ,uhifadhi wa mizigo ,uhudumiaji wa makontena ,matenki ya mafuta n,k |
Halmashauri ya Mji Korogwe imetenga viwanja vitatu kwa ajili ya Bandari Kavu. eneo hilo liko katika Kata ya Old Korogwe Mashariki ya Korogwe. Eneo la kwanza lina ukubwa wa Hekta 3.6 lipo kwenye nyuzi 38° 29’ E na 5º 09’ S. Eneo la pili lina ukubwa wa Hekta 14.8 lipo kwenye nyuzi 38° 29’ 30’’ E na 5º 09’ S. Na eneo la tatu lina ukubwa wa Hekta 17.93 lipo kwenye nyuzi 38° 29’ 45’’ E na 5º 09’ S. Umbali kutoka kwenye kila eneo hadi kwenye njia ya reli ni mita 25. Umbali kutoka bandari ya Tanga ni kilometa 94, na kuelekea Dar es salaam ni kilometa 350. Kwa upande wa magharibi kuna mtandao wa barabara unaounganisha Mnyuzi na wilaya ya Muheza. Pia eneo linapitiwa na reli ya Tanga, Dar es salaam Arusha.
|
Eneo limetengwa, taratibu za ulipaji fidia na upatikaji wa hati zinaendelea
|
Huduma za kuwezesha uwekezaji kama umeme, maji na mawasiliano zipo karibu na eneo hili.
|
|
2
|
VIWANDA:
1.Usindikaji wa Mazao ya kilimo na mifugo |
Eneo la mita za mraba 9000 limetegwa kwa ajili ya viwanda vidogo na vya kati katika kata ya Old Korogwe(Industrial park)
|
Eneo limetengwa, taratibu za ulipaji fidia na upatikaji wa hati zinaendelea
|
Malighafi zinapatikana kiurahisi ndani na nje ya Mji wa Korogwe kama
- matunda ya aina mbalimbali. -Mazao ya misitu. Mazao ya kilimo (Mkonge,Mpunga na Mahidi n.k -Mazao ya mifugo kama Nyama,Ngozi,Mifupa . |
|
2. EPZ na Uwekezaji wa viwanda mbalimbali .
|
Eneo la hekta 2000 limeainishwa na kutengwa katika kata ya Mgombezi kwa ajili ya EPZ (Export processing zone) na uwekezaji wa viwanda mbalimbali.
|
Utaratibu wa kubadilisha matumizi na kulipima eneo hili unaendelea ili liwe na hati ya umiliki
|
Eneo hili lipo karibu na mnada wa mifugo ,linafikika kiurahisi na huduma muhimu zipo karibu.
|
||
3
|
UTALII:
Hoteli,Maeneo ya burudani na maeneo ya biashara |
Maeneo yenye ukubwa wa Hekta 10 na Hekta 2.6 kwenye eneo lenye nyuzi 38o 27’ 45” E na 5o 09’ S yametengwa katika kata ya Old Korogwe kwa ajili ya mahoteli na biashara.
|
Eneo limetengwa, taratibu za ulipaji fidia na upatikaji wa hati zinaendelea
|
Kuna uhitaji Mkubwa wa huduma hii kwani semina na mikutano mbalimbali inafanyika katika Mji wetu.
|
|
4
|
ELIMU:
Chuo kikuu /Chuo cha ufundi |
Eneo la uwekezaji kwa taasisi za elimu lipo kata ya Old Korogwe Lina ukubwa wa Hekta 42 na liko kwenye nyuzi 38° 29’ E and 5º 09’ S.
|
Eneo limetengwa, taratibu za ulipaji fidia na upatikaji wa hati zinaendelea
|
Mahitaji makubwa katika ngazi zote za elimu.
Eneo lipo katika mazingira mazuri ya utoaji Elimu. |
|
5.
|
MICHEZO:
Kiwanja cha michezo cha kimataifa na shule ya michezo |
Eneo lenye ukubwa wa Hekta 13 limetengwa katika Kata ya Old Korogwe Kwazomolo
|
Eneo limetengwa taratibu za upimaji zinaendelea ili liwe na Hati ya umiliki.
|
Mji wa Korogwe una uhitaji Mkubwa wa viwanja vya kisasa vya michezo na chuo cha michezo ili kukuza vipaji vya vijana .
|
|
6
|
UJENZI :
Ujenzi wa nyumba za makazi na biashara |
Halmashauri ya Mji imepima na inampango wa kupma viwanja katika kata ya Bagamoyo , maeneo ambayo yanafaa katika ujenzi wa nyumba za kuishi, biashara na upangishaji .
|
Maeneo yaliyopimwa yanatolewa hati ya umiliki
|
Maeneoyanayopimwa yanakuwa karibu na huduma muhimu na barabara zinachongwa.
|
|
|
|
|
|
||
|
|
||||
|
|
|
|
|
|
Halmashauri ya Mji Korogwe inawakaribisha muweze kuwekeza katika fursa zilizopo katika Mji wetu .
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.