Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope amewakabidhi wanakikundi cha Mshikamano fund Idara ya Kilimo Kompyuta Mpakato (Laptop) kumi zenye thamani ya Shilingi Milioni Tano na Laki mbili (5,200,000).Bi. Mwashabani Mrope amekabidhi Kompyuta Mpakato hizo kwa Kikundi cha mshikamano Idara ya Kilimo kwa lengo la kuimarisha ufanisi wa kazi wakati wakitekeleza majukumu yao na pia itadumisha upendo na mshikamano mahali pa kazi. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Septemba 10, 2025 (Mwaka huu) katika ofisi za uthibiti ubora wa Shule Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Bi. Mwashabani Mrope aliwaasa wanamshikamano pasitokee hata mtu mmoja atakayewakatisha tamaa katika umoja wenu pendaneni ili kikundi kiweze kusonga mbele hata wale waliohama watamani kurudi tena”alisema Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe”pia Bi. Mwashabani Mrope alichangia kikundi cha Mshikamano fund fedha za kitanzania Shilingi Laki mbili ili kutunisha mfuko huo. Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano fund Bw.Hamis Kileta alifafanua kuwa kikundi hiki lengo lake kuu ni kusaidiana wakati wa shida na wakati wa raha. Aliendelea kwa kumshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kutukabidhi Kompyuta Mpakato Pamoja na kututia moyo na tunakuhaidi tutashikamana na kupendana.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.