Halmashauri ya mji wa Korogwe ina vivutio vingi vya utalii ambapo uekezaji ukifanyika utaleta tija kubwa kiuchumi.Fursa hizi ni nadra sana kupatikana sehemu nyingine kutokana na uhalisia wake.Vifuatavyo ni orodha ya vivutio vilivyopo ikianisha jina la kivutio,mahali kilipo,sifa zake pamoja na jinsi ya kukifika kwa maana ya njia.
NA.
|
JINA LA KIVUTIO
|
MAHALI KILIPO
|
SIFA ZAKE
|
HALI YA BARABARA
|
1.
|
KISIWA CHA MAKAZI YA MAMBA
|
Mtaa wa Old Korogwe katika Kata ya Old Korogwe
|
Eneo limezungukwa na Maji ya Mto Pangani, lina ukubwa wa Hekta 3.5, ni mapunziko ya wanyama waishio ndani ya Maji wakiwemo mamba.
Ukiwa ndani ya kisiwa utapata upepo mzuri. Ni kivutio cha Kiikolojia. |
Hufikika kwa kutumia Mitubwi ya wenyeji wa maeneo ya Old Korogwe.
|
2.
|
KIVUKO CHA CHIFU MBEGA WA USAMBARA
|
Mtaa wa Msambiazi katika Kitongoji cha Gudisheni Kata ya Mtonga.
|
Eneo la Mto Pangani ambapo Chifu Mbega wa Usambara alitumia kuvuka mto wakati akiwakimbia Maadui zake, ni sehemu nyembamba ya eneo pana la Mto.
Ni kivutio cha kihistoria. |
Eneo hili hufikika katika kipindi chote cha majira kwani kipo pembezoni mwa barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kuelekea mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
|
3.
|
KILELE CHA MLIMA FUNDI
|
Mitaa ya Masuguru, Makwei, Old Korogwe na mlima Fundi katika Kata za Manundu, Masuguru, Magunga na Old Korogwe.
|
Uwapo kwenye kilele cha mlima huu utaweza kuona eneo lote la kati ya Mji wa Korogwe. Utaweza kuona pango la asili ambalo lina maji ya siyo kauka, kuna hali ya baridi. Wanyama wadogo wa asili wanaishi,
Ni kivutio cha kipekee. |
Hakuna barabara, ya kupanda mlimani, kunafikika
kwa njia za miguu. |
4.
|
MITAMBO YA MKONGE NGOMBEZI SISAL ESTATE
|
Mtaa wa Matondoro katika Kata ya Ngombezi
|
Ni mitambo inayozalisha umeme ya enzi za ukoloni, eneo ambalo umeme unazalishwa kwa kutumia mabaki ya mkonge.
Ni kivutio cha kipekee. |
kunafikika kipindi chote cha Majira ya mwaka kwa njia ya barabara na reli.
|
5.
|
MNARA WA MSUMBIJI KILOLE
|
Mtaa wa Kilole Manzese katika Kata ya Bagamoyo
|
Ni eneo lenye mnara wa nchi ya Msumbiji ambapo palikuwa na ofisi ya Chama cha Frelimo cha wakazi wa Msumbiji waishio Tanzania, Palikuwa ni kituo cha kupiga kura wakati wa uchaguzi wa kwanza wa Rais wa Msumbiji.
|
Barabara ni ya Lami pembezoni mwa Barabara kuu ya Dar es Salaam kuelekea Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
|
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.