KIWANDA CHA KUSINDIKA MAZIWA
Katika eneo la Halmashauri ya mji wa Korogwe tu kunaziada ya maziwa inayofikia wastani wa lita 12000 kwa mwaka.Pamoja na hayo ifahamike kuwa ziko Halmashauri nyingine jirani kama vile Handeni,Bumburi,Korogwe vijijini pamoja na Lushoto ambazo pia ni wafugaji wazuri.Ikiwa kiwanda kinawekwa Korogwe mjini, ni rahisi pia kukusanya maziwa kutoka wilaya hizi majirani kwani Korogwe mji ipo katikati ya Wilaya hizi.Katika Mkoa mzima wa Tanga kipo kiwanda kimoja tu cha kusindika maziwa hivyo ni fursa kwa yeyote aliye tayari kuwekeza kwani asilimia kubwa ya wakazi wa Mkoa wa Tanga pia ni wafugaji.
KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI
Bidhaa zitokanazo na ngozi zimeonekana kuwa na umuhimu mkubwa sana kwa sasa.Ikizingatiwa kwamba kwa Korogwe mjini tu kuna zaidi ya ngozi 3000 za ng’ombe na ngozi 14000 za mbuzi kwa mwaka.Pia kwa kanda hii kaskazini kuna kiwanda kimoja tu kinachofahamika cha kuchakata ngozi hivyo ni fursa iliyo dhahiri kuichangamkia kwa hapa Korogwe mjini.Uwekezaji unaweza kua ni wakiwango cha kuhudumia wateja wadogowadogo na kuhudumia viwanda vingine vikubwa zaidi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.