• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Mji wa Korogwe
Halmashauri ya Mji wa Korogwe

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Korogwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Ardhi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi waJamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
    • Mifugo
    • Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Za afya
    • Kielimu
    • Za Maji
    • Za kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Elimu, afya,uchumi na maji
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Picha za Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

MWIGULU AFURAHISHWA NA MRADI WA MAJI KOROGWE

Posted on: February 14th, 2026


Na Mwandishi wetu- Korogwe Februari 14, 2026,

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ametoa pongezi alipokagua Mradi wa Maji wa Miji 28 uliopo Kata ya Mswaha Wilayani Korogwe  Mkoa wa Tanga utakaohudumia miji ya Korogwe, Muheza, Pangani na Wilaya ya Handeni.  Mradi huo utakapokamilika utafanikiwa kuhudumia wananchi 860,000.

Amesema pongezi ziende kwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo ni matokeo ya nia na dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuwatumikia Watanzania kupitia utoaji huduma kwa maendeleo na ustawi wa watu, na kuongeza kuwa mradi huo utaupa heshima Mkoa wa Tanga, na kuleta tija kwa wananchi kuweza kupata maji.

Naye Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso, alisema mradi huo unaosimamiwa na Handeni Truck Main (HTM), utagharimu Shilingi bilioni 171, alisema mradi huo umetokana na mradi uliokuwepo awali wa Handeni Trunk Main (HTM) uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GTZ) na sasa GIZ mwaka 1974 ulikuwa na uwezo wa kutoa lita za ujazo milioni 4 kwa watu 180,000


Wananchi wa wilaya hizo wamefurahishwa na mkakati wa serikali kwa ujenzi wa mradi huo.

AKAMATWE

WAZIRI Mkuu, Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kusakwa na kuwekwa ndani Mkurugenzi wa kampuni ya Greens Construction Limited, Hamimu Kusaga, anayedaiwa kulipwa Shilingi milioni 934 za mradi wa ukarabati na upanuzi wa katika mji mdogo wa Mombo, kisha kuutelekeza.

Mhe Dkt Mwigulu amesema, mkandarasi huyo anayedaiwa kuishi jijini Dodoma atakapopatikana, anapaswa kusakwa, kukamatwa na kuwekwa ndani hadi atakaporejesha fedha hizo, kisha hatua nyingine za kisheria kuchukuliwa.

Ili kufanikisha azma hiyo, Mhe Dkt. Mwigulu, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt. Batilda Burian, kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe Rosemary Senyamule, ili mkandarasi huyo akamatwe na kufikishwa Korogwe.

“Fedha za umma si kama matunda ya porini ambayo kila mtu anapita na kuchuma na kuondoka zake...haya ndio mambo yasiyovumilika,” amesema.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe William Mwakilema, alisema mtuhumiwa huyo alilipwa fedha hizo kwa kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita, na mchakato wa kumfungulia mashtaka unaendelea.

Akizungumzia mradi wa maji miji 28, Mhe Dkt. Mwigulu amesema ni matokeo ya nia na dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuwatumikia Watanzania kupitia utoaji huduma kwa maendeleo na ustawi wa watu.

Mhe Dkt Mwigulu alielekeza, kutokana na matokeo ya dhamira hiyo inayoonekana pia kwenye miradi mingine nchini, watu wasimame kama ishara ya kumheshimisha Mhe Rais Dkt. Samia, ikawa hivyo.

Naye Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso, alisema mradi huo unaosimamiwa na Handeni Truck Main (HTM), utagharimu Shilingi bilioni 171 na kuwanufaisha wakazi wa wilaya za Korogwe, Muheza na Pangani.

Amesema, awali, mradi huo wenye miundombinu iliyojengwa mwaka 1974 na kuwa chakavu, ulikuwa na uwezo wa kutoa lita za ujazo milioni 4 kwa watu 180,000 ,lakini utakapokamilika utatoa lita za ujazo milioni 52 kwa siku, ukiwanufaisha watu 860,000.

Wananchi wa wilaya hizo, wamepongeza jitihada za Serikali kufanikisha mradi huo utakawaondoa kwenye kadhia ya ukosefu wa maji ya uhakika

Matangazo

  • ERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN KOROGWE TOWN UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KLINIKI YA ARDHI KOROGWE MJI August 11, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI October 06, 2025
  • UWEPO WA FEDHA TSH. 100,000.000/= KUVIKOPESHA VIKUNDI. January 21, 2026
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MWIGULU AFURAHISHWA NA MRADI WA MAJI KOROGWE

    February 14, 2026
  • TATHMINI YA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2025

    February 07, 2026
  • MADIWANI WAONYESHA HAMASA KUFUATILIA MIRADI

    February 04, 2026
  • URAHISISHAWJI KAZI ZA MIFUGO

    February 02, 2026
  • Angalia Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa Muhimu

  • Ukodishaji wa Ukumbi
  • Ukasanyaji wa Taka

Tovuti Zinazohusiana

  • TOVUTI YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • MKOA TANGA
  • TUME YA AJIRA
  • PPRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Korogwe Tanga Tanzania

    S.L.P: 615 Korogwe

    Simu: 0272650050

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.