MRADI WA KITUO CHA MABASI CHA KISASA KOROGWE
Korogwe ni kitovu muhimu cha biashara na huduma zakijamii kwa wasafiri wa ndani ya Korogwe na wasafiri wa kati ya Mikoa ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro Dar Es Salaam, Mbeya, Iringa,Morogoro, Nairobi, na Kampala kutumia barabara kuu ya Dar Es Salaam Arusha na Tanga Arusha.
Kituo cha kisasa cha mabasi kimejengwa Korogwe Mjini karibu na mzunguko wa makutano ya barabara ya Dar Es Salaam Arusha na Barabara iendayo Wilaya ya Handeni kikiwa na uwezo wa kuhudumia mabasi makubwa 45 na madogo 33 kwa wakati mmoja na jumla ya mabasi 15 yafanyayo safari za ndani na nje ya nchi kwa wakati mmoja.
Kituo kimezungukwa na maduka 121 yanayotoa huduma mbalimbali za kijamiii kwa wasafiri na wananchi wa Mji wa Korogwe na sehemu ya kuegesha magari ya wanunuzi iliyo na vituo 15
Mradi wa kituo kikuu cha mabasi umekamilika tangu mwaka jana 2017 na kuzinduliwa na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Jonh Joseph Pombe Magufuli.Hata hivyo mradi huu umekua mojawapo ya vitega uchumi vikubwa vya halmashauri kwani kila mwezi wastani wa fedha za kitanzania milioni thelathini hukusanywa.Fedha hizi hutumika kutekeleza huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchangia ujenzi wa barabara,miundo mbinu ya maji,elimu pamoja na afya.Pia hutumika kuwawezesha kina mama na vijana kupitia vikundi vya ujasiriamali.Kwa ujumla mradi huu uligharimu jumla ya fedha za kitanzania bilioni nne ambazo zilifadhiliwa na Benki ya Dunia.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.