Kampeni ya Vijana Mtaa kwa Mtaa ni kampeni iliyoandaliwa na kuratibiwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Afisa wa Vijana Halmashauri ya Mji wa Korogwe ikiwa na lengo la kuelekeza,kukwamua vijana kiuchumi na kijamii. Kampeni hiyo ina lengo la kuibua changamoto za vijana, kuwapa elimu vijana na kuwaelekeza mbinu mbalimbali za kuinua uchumi pamoja na namna ya kuanzisha, kusajili vikundi na kupata mikopo na fursa mbalimbali zinatolewa na Halmashauri ya Mji Korogwe.
Kampeni ya Vijana Mtaa kwa Mtaa ilianza Disemba 13, 2025 na kumalizika katika Mtaa wa Kitifu Januari 7, 2026 ikiwa na kauli mbiu “Vijana na Maendeleo”. Katika kampeni hiyo vijana wamepata mafunzo mbalimbali yakiwemo:-
>Kufahamu namna ya kuanzisha,kusajili kikundi kwajili ya kupata mkopo wa vijana 10% inayotolewa na Halmashauri.
>Ujuzi wa ujasiriamali,kilimo na kuboresha biashara zao kidigitali.
>Fursa za mikopo inayotolewa na Halmashauri pamoja na Taasisi za Kifedha ziliopo Korogwe Mji.
>Mpango mkakati uliowekwa na Halmashauri ya Mji kwa ajili ya kuinua vijana kiuchumi.
>Elimu juu ya namna ya kupata vitambulisho wa ujasiriamali na umuhimu wake.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Happy Luteganya amewataka vijana kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Mji ili kujikwamua kiuchumi.
Naye Afisa Vijana Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Rajabu Dimosso amewataka vijana kutumia fursa walizowezeshwa ili kuleta tija katika kujikwamua kiuchumi na kijamii. Aidha amewasisitiza vijana kuwa chachu ya kuibua vitendo vya uvinjufu wa amani katika Mitaa yao na kuwa mbele katika kutaka maendeleo na kutumia vema mitandao ya kijamii.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.