UTANGULIZI
Idara ya Ujenzi ni mojawapo ya idara katika Halmashauri ya Mji Korogwe, inayofanya kazi kwa mujibu wa sheria ya uanzishwaji wa serikali za mitaa.
Idara ya Ujenzi imegawanyika katika sehemu tatu,
1.Sehemu ya Barabara
2.Sehemu ya Majengo
3.Sehemu ya Mitambo na Umeme
MAJUKUMU YA IDARA
1.Kusimamia ujenzi na Ukarabati wa majengo yote ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
2.Kusimamia matengezo ya magari ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
3.Kufanya tathimini ya miundombinu ya barabara za Mji wa Korogwe na kufanya makadirio ya gharama za matengenezo
4.Kusimamia wakandarasi wote wanaofanya kazi za ujenzi katika miradi ya Halmashauri.
KUBORESHA BARABARA
•Kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuweza kuboresha barabara za mji kwani kwa sasa Halmashauri inategemea vyanzo viwili tu ambavyo ni makusanyo ya ndani na Mfuko wa Barabara.
•Kuelimisha jamii umuhimu wa kushiriki kulinda miundombinu ya barabara.
•Kuelimisha Jamii kuepuka kuvamia maeneo ya hifadhi ya barabara.
•Kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili waache kutupa takataka ngumu kwenye mifereji ya maji ya mvua
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.