Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Zahara Msangi afanya kikao na wafanyabiashara wa Korogwe kwa lengo la kujadili namna ya ulipaji wa mapato na kuendeleza Mji wa Korogwe.Kikao hicho kimefanyika Disemba 12, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe kikiwa na lengo la kuweka maazimio ya ulipaji ushuru wa huduma(Service Levy).
Katika kikao hicho Bi. Zahara amewataka Wafanyabiashara kuwa chachu ya maendeleo ya Mji wa korogwe, kwa kulipa ushuru wa huduma ambao ni 0.25% ya mauzo yao. Bi. Zahara alisema kuwa “Mimi kama Mkurugenzi kazi yangu ya kwanza ni kuleta maendeleo ya Korogwe” hivyo nawaomba mkawe mabalozi kwa Wafanyabiashara wengine katika kuhakikisha wanalipa mapato, kwani mapato hayo ndio maendeleo ya Korogwe.
Aidha Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Bw. Lyamuya amemshukuru Mkurugenzi kwa kuwaita na kuweka mikakati ya pamoja juu ya ulipaji wa madeni yao ya ushuru wa huduma na kusema kuwa wako tayari kulipa. Pia ameiomba Serikali kuweka utaratibu mzuri wa malipo ya ushuru wa huduma ili waweze kulipa madeni yao ya nyuma kwani wanaamini kuwa Serikali inataka wao pia wakuwe kiuchumi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.