MAJUKUMU YA IDARA:
Kuratibu shughuli zote za usimamizi na uendelezaji wa Miji ikiwa ni upangaji wa Mji, Upimaji wa Ardhi, uthaminishaji na umilikishwaji kwa mujibu wa sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 na sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007.
Idara ya Mipango Miji na Ardhi hutoa huduma kwa wananchi kupitia vitengo vyake vikuu vinne;-
KITENGO CHA MIPANGO MIJI.
Kuratibu shughuli zote za usimamizi wa uendelezaji wa Mji wa Korogwe.
Usimamizi na uendelezaji Miji unahusisha upangaji wa matumizi ya Ardhi na urasimishaji wa makazi yasiyo rasmi.
Kutoa elimu na ushauri kwa jamii kuhusu uendelezaji Mji kwa mujibu wa sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007.
KITENGO CHA ARDHI.
Kusimamia masuala yote ya ardhi ikiwa ni uaandaaji wa hatimiliki, uhamisho wa miliki, na utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Kusikiliza migogoro ya ardhi kwenye Kata na kuitafutia ufumbuzi.
Ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali ikiwemo kodi ya pango la ardhi (Land Rent).
Inashughulikia masuala yote ya uthamini, ikiwemo uthamini kwa ajili ya fidia, uthamini kwa ajili ya kodi za majengo, uthamini kwa ajili kubadili miliki na ukadiriaji wa kodi ya majengo, Ardhi pamoja na malipo ya mbele ya ardhi. (Premium), uthamini kwa ajili ya dhamana, uthamini kkwa ajili ya kuongeza muda wa kumiliki hati (Renewal).
KITENGO CHA UPIMAJI NA RAMANI.
Kinashughulikia shughuli zote za upimaji wa ardhi na uandaaji wa ramani za upimaji (Survey plans)
Kuonyesha mipaka ya viwanja.
Kuandaa na kusaini ramani za hati (deed plans)
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.