Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bw. Burhani Ngulungwa amewataka vijana katika Halmashauri ya Mji Korogwe kuchangamkia fursa za vijana zinzotolewa na Halmashauri, Serikali kuu pamoja na Wadau wa Maendeleo.
Kaimu Mkurugenzi huyo aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku Moja kwa viongozi wa vijana katika mitaa 29 ya Halmashauri ya Mji Korogwe Januari 30, 2026. Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao yalifanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe na kuhudhuriwa viongozi wa vijana kutoka katika 29 iliyopo katika Mji wa Korogwe, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata na Wadau wa Maendeleo.
Aidha Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Korogwe Bi Happy Luteganya amewaasa Viongozi hao kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wenzao kwani wamewaamini na kuwachagu kuwa wawakilishi wao.Pia amewataka kufanya kazi kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali katika ngazi za Mitaa na Kata ili kuwa na taarifa sahihi zinazohusu Maendeleo ya Vijana kutoka Serikalini.
Naye Afisa Vijana wa Halmashauri Ndg Rajab Dimosso amewataka Vijana hao kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kuwaletea tija katika ustawi wa shughuli zao za kijamii, kiuchumi na kutokukubali kutumika katika uvunjivu wa Amani na Utulivu wa Nchi yetu.
Kampeni ya ziara ya kuzungumza na Vijana katika Mitaa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mheshimiwa Joel Arthur Nanauka kwa mamlaka za Halmashauri kuhakikisha vijana wanasikilizwa na kutatuliwa changamoto zao kwa wakati, ili kuendana na kasi ya Wizara yake katika kutafsiri maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuleta Maendeleo ya Vijana ambao wanakadiriwa kufikia asilimia 34 ya Watanzania wote.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.