Upanuzi wa kituo cha afya cha majengo
Halmashauri ya mji wa Korogwe imepata neema ya upanuzi wa kituo chake cha afya kupitia Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo inajumuisha ujenzi wa jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, nyumba moja ya mtumishi, maabara pamoja na jengo la mionzi.
Ujenzi umeanza mwezi wa sita 2018 na unatarajiwa kumalizika mnamo mwezi wa kumi na moja 2018.Mradi umeshakamilika kwa kiasi cha 50% hadi sasa.Unatekelezwa na Serekali chini ya Ofisi ya Raisi TAMISEM na utagharimu jumla ya milioni 500 ambazo tayari zimeshatengwa.Hata hivyo upanuzi wa kituo hiki utawezesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi wote wa Halmashauri ya mji wa Korogwe na Halmashauri majirani.
Ujenzi wa Miundombinu ya maji ya Msambiazi, Lwengera relini na Lwengera darajani
MSAMBIAZI
Mradi huu umeanza tangumwezi wa tisa 2017 na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi wa sita mwaka huu.Umeshakamilika kwa kiwango cha 75% kwani ujenzi wa tanki kubwa pamoja na vilula tayari;ulazaji wa mabomba unaendelea kwa sasa. Wafadhili wa mradi ni WSDP yaani benk ya Dunia na utagharimu fedha za kitanzania zipatazo 761,475,594.Mradi kwa sasa upo hatua za ukamilikaji.Utakapokamilika unatarajiwa kufanikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa mji wa korogwe. Chanzo kikuu cha maji ni kutoka mto Pangani.
LWENGERA
Mradi huu umeanza tangumwezi wa kumi na mbili 2017 na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi wa sita mwaka huu.Umeshakamilika kwa kiwango cha 15% kwani ujenzi wa awali unaendelea kwa sasa. Wafadhili wa mradi ni WSDP yaani benk ya Dunia na utagharimu fedha za kitanzania zipatazo 76,475594.Utakapokamilika unatarajiwa kufanikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Lwengera relini na Lwengera darajani pamoja na maeneo ya old Korogwe.Chanzo kikuu cha maji ni kutoka mto Pangani.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.