Shule Mpya ya Sekondari Majengo ni miongoni mwa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali kuipitia Programu ya uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) iliyogharimu zaidi ya shilingi Milioni mia Tano(584,280,029) iliyolenga kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule za Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Kukamilika kwa mradi huu kumepunguza mwendo kwa wanafunzi wanaoishi maeneo ya Old korogwe pamoja na Kata ya Majengo kwani kabla ya uwepo wa shule hii wanafunzi waishio kata ya Majengo walizimika kusoma katika shule za Nyerere na Old Korogwe ikiwa ni umbali wa zaidi ya Kilomita 1 kutoka wanapoishi.
Shule hiyo imepokea Wanafunzi 106 kati yao wavulana wakiwa 51 na wasichana 55 baada ya miundombinu ya madarasa nane,matundu 8 ya vyoo vya wanafunzi,jengo la utawala lenye ofisi 5 pmaoja na matundu 6 ya vyoo vya walimu,maabara 2 kukamilika, viti na meza za Wanafunzi na Walimu zikiwa tayari.
Licha ya kupunguza mwendo katika mchakato wa ukamilishaji wa mradi huu zaidi ya ajira 50 zilitolewa na kuwanufaisha wakazi wa kata ya majengo na Korogwe kwa ujumla.
Katika ajira hizo wafanyabiashara, wenye Vyombo vya usafirishaji na mafundi walinufaika na kujikwamua kiuchumi.
"Asante Serikali ya awamu ya sita kwatupa fursa na faraja kwa kupunguza mwendo kwa watoto wetu, kutupa ajira na fursa ya kibiashara"
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.