Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mary Stephen Mmary kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope amewataka Maafisa Elimu kata, Wakuu wa Shule, Walimu wakuu Pamoja na wadau wa Elimu kuendeleza Elimu ya Watu wazima kwani Elimu hii inasaidia kupata matokeo ya moja kwa moja ya uzalishaji yanatokea hapo kwa hapo tofauti na Watoto ambao wako katika m fumo rasmi. Bi. Mary Mmary ameyasema hayo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Juma la Elimu ya Watu wazima kwa ngazi ya Halmashauri iliyofanyika Katika ukumbi wa Shule ya Msingi New Korogwe Sptemba 8 (mwaka huu) 2025.
Naye Afisa Elimu Watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi Msingi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Aseri Stephano Mshana alisema” Kujifunza kwa watu wazima umejikita katika ukweli kwamba watu wazima ndio wazalishaji wa moja kwa moja hivyo wakipewa Elimu yenye ubora matokeo yake ni makubwa na uzalishaji wake unatokea hapo kwa hapo tofauti na Watoto ambao ni Taifa la kesho”.Bw. Mshana aliendelea kufafanua kuwa hapa Tanzania Elimu ya Watu wazima ilianza rasmi mwaka 1975 ambapo baada ya uhuru ilionekana Watu wenye Elimu ni wachache kuweza kuendeleza Sera ya Azimio la Arusha ya ujamaa na kujitegemea.Katika utekelezaji wa Elimu ya watu wazima, program mbalimbali ziliundwa ikiwemo SEQUIP,MUKEJA na OPEN SCHOOL kwa ajili ya kusaidia elimu ya watu wazima. Kitaifa Juma la Elimu ya Watu wazima itaadhimishwa Mkoani Katavi kuanzia Septemba 15 hadi Septemba 20, 2025. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo yanasema”Kukuza kisomo katika zama za kidigitali kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.