Kufuatia kikao cha Waheshimiwa madiwani kilichofanyika leo tarehe 27/04/2018 katika ukumbi wa halmashauri, taarifa ya mapato na matumizi imeonesha kwamba; mapato yote kwa jumla yalikua TSH 3,985,862,280.98 na matumizi kiasi cha TSH 4,389,954,130.03 kwa kipindi chote cha kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa tatu mwaka huu.
Hata hivyo mapato hayo yanajumuisha ruzuku mbalimbali zenye jumla ya TSH 3,698,854,431 kutoka serekali kuu na wadau wa maendeleo pamoja na makusanyo ya vyanzo vya ndani yanayofikia jumla ya 237,007,849.76.Pia matumizi hayo ni pamoja na kiasi cha TSH 1,187,926,592.44 zilizotumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na kiasi cha TSH 2,797,935,689 zilitumika katika kuendesha ofisi pamoja na kulipa mishahara ya watumishi na pasho za Waheshimiwa madiwani.
Baraza hilo pia limepitia na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji kazi wa kamati zote za kudumu na kutoa maelekezo stahiki yenye kulenga kuboresha huduma za jamii ya Wanakorogwe mji na Taifa kwa ujumla.Baadhi ya taarifa hizo ni za Kamati ya mipango miji na mazingira,Fedha na utawala,Kudhibiti ukimwi,Elimu,afya,maji na uchumi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.