Kikao cha baraza maalumu la Madiwani kupitia na kutoa maoni juu ya hoja za Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kimefanyika tarehe 29/06/2017 na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martine Shegella ambapo katika kikao hicho hoja mbalimbali zilijadiliwa na kutolewa maoni hasa ikiwa ni kuhakikisha hoja hizo zinajibiwa kwa ufasaha na hazijirudii tena katika ukaguzi ujao wa mwaka wa fedha 2016/2017.
Aidha katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga alipata fursa ya kutoa neno na kuitumia nafasi hiyo kuipongeza timu nzima ya wataalamu wa Halmashauri ya Mji Korogwe na ofisi ya Mkuu wa Wilaya Korogwe kwa namna ambavyo wamekuwa wakitekeleza miradi kwa haraka nmo, amepongeza uwekezaji mkubwa uliofanyika wa stendi mpya na yakisasa inayoiletea sifa Halmashauri na Mkoa wa Tanga kwa ujumla.
Akizungumza katika kikao hicho katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bi. Zena A. Said alishauri wataalamu kuwa makini katika kutunza kumbukumbu mbalimbali za mahesabu ya Halmashauri na kuzingatia uwepo wa viambatanisho vyote muhimu kabla ya kufanya malipo, pia alisistiza kutenga pesa kwa ajili ya kutoa mkopo kwa vikundi vya kina mama na vijana na kuwafatilia ili mikopo hiyo iweze kurudi na iwe yenye tija kwa vikundi hivyo na kwa Serikali.
Naye Mkuu wa Wilaya Korogwe aliwashukuru timu ya wataalamu wa Halmashauri ya Mji Korogwe wakiwemo watendaji wa Kata kwa jinsi wanavyompa ushirikiano katika miradi mbalimbali anayoianzisha kwa njia ya msalagambo na kuwaahidi zawadi nono kwa mtendajia ambaye kata yake itafanya vizuri.
Madiwani wakifatilia kwa Makini taarifa ya Hoja
Mkuu wa Wilaya Korogwe akitoa neno.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.