Maafisa mifugo kutoka kata mbalimbali za Halmashauri ya Mji wa Korogwe wameendesha zoezi la uchanjaji wa mbuzi, Chanjo hiyo imetolewa kuwakinga Mbuzi dhidi ya ugonjwa wa Sotoka (PPR). Zoezi la uchanjaji lilifanyika Oktoba 1, 2025 katika Kata ya Kwamsisi Mtaa wa Kwakombo Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Lengo kuu la chanjo hiyo ni kuwakinga Mbuzi dhidi Sotoka (PPR). Jumla ya Mbuzi waliochanjwa ni 160 kwa siku. Halmashauri ya Mji wa Korogwe inaishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.