Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi amempongeza Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushika nafasi ya pili katika utoaji mikopo asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi huyo kwa Bi. Happy Luteganya Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii baada ya kuwasilisha cheti cha pongezi kilichotolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika majumuisho ya kikao kazi kila Jumatatu(Morning Prayer) kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Novemba 17, 2025.
Katika mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Tsh 437,755,116.90 kwa vikundi 66 vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 sawa na asilimia 101 kwa mwaka.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.