Mratibu wa Dawati la Mtoto Halmashauri ya Mji wa Korogwe ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Amina Fundi akiambatana na Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Mtonga Bi. Zuhura Njemo amefanya ziara katika Shule ya Msingi Mtonga kata ya Mtonga. Lengo ya Ziara hiyo ni kutoa Elimu ya Ukatili wa Kijinsia na Maadili kwa Watoto. Watoto wameaswa kutoa Taarifa wanapoona Viashiria Vya vitendo vya ukatili katika maeneo yao kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola vilivyopo karibu au kwa walimu na mtu unayemwamini. Ziara hiyo imefanyika Julai 16 (Mwaka huu) 2025 katika Shule ya Msingi Mtonga.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.