Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. William Mwakilema amewataka Maafisa Ugani Mifugo wote katika Halmashauri ya Mji Korogwe kuhakikisha mifugo yote inachanjwa Kama muongozo unavyosema. Mh. Mwakilema alitoa kauli hiyo wakati wa Kampeni ya Kitaifa ya Utambuzi na Uchanjaji wa Mifugo. Zoezi hilo lilifanyika Julai 10, 2025 Kwa Mfugaji Bi. Zaina Kileo Mtaa wa Manzese Kata ya Bagamoyo.
Mkuu wa Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Ramadhani Sekija “alieleza kuwa Halmashauri kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepokea Chanjo pamoja na Vifaa wezeshi kwa ajili ya zoezi la Chanjo kwa Mifugo ya Kuku, Mbuzi na Ng’ombe.
Chanjo na Vifaa wezesheji zilizotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni pamoja na Chanjo ya Tatu moja dozi 40,000 dhidi ya Kideri, Ndui na Mafua ya Kuku,Chano dozi 4000 ya Ng’ombe dhidi ya Homa ya Mapafu (CBPP) na Chanjo dozi 8,900 ya Mbuzi dhidi ya Sotoka (PPR). Kwa upande wa Vifaa wezeshi ni Mabuti jozi 10, Sindano 116, Mabomba ya sindano4, Nguo za kufanyia kazi (overoll) 10, Hereni za kuvalisha Ng’ombe 4000, Box za kupoozea (Cool boxes). Bw. Sekija ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwapatia vifaa wezeshi pamoja na Chanjo kwani itasaidia kukinga mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.