Halmashauri ya Mji wa Korogwe yakabidhiwa Mafuta kwa ajili ya Wanafunzi wenye ulemavu wa Ngozi (Ualbino) kutoka Kikundi cha Matendo ya Huruma.Mafuta hayo yamepokelewa na Afisa Elimu Maalumu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Hiyana Mlawa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mafuta hayo yenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni moja na Laki Nane (1,800,000.00) yamekabidhiwa kwa Mtoto Hadija Bakari akiwakilisha Watoto wengine wenye Ulemavu wa Ngozi (Ualbino) katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe Machi 26, 2025.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.