Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Balozi Dkt. Batilda Burian ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kupata Hati safi kutoka kwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ukusanyaji mzuri wa Mapato kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa Asilimia 98 na kuwa Halmashauri ya kwanza kuvuka lengo kati ya Halmashauri 11 za Mkoa wa Tanga. Mh Balozi Dkt. Batilda Burian ametoa pongezi hizo katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kupitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Juni 13, 2025.
Kwa upande mwingine Mh.Dkt. Batilda alifafanua watumishi msaidieni Mkurugenzi pamoja na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutatua changamoto za wananchi ikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato na kusimamia mifumo ya Serikali vizuri wakati wa kutekeleza majukumu. Katika Kikao hicho Dkt. Batilda Burian aliagiza Menejimenti chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kuhakikisha hoja zote za Ukaguzi zilizowasilishwa zinatekelezwa kikamilifu ifikapo Juni 30, 2025
Katika Kikao hicho kilihudhuliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Pili Mnyema, Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na ya Wilaya, Maafisa kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji kata kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.