Halmashauri ya Mji wa Korogwe yatoa mkopo wa Shilingi Milioni Mia Mbili na Hamsini
Halmashauri ya Mji wa Korogwe imekabidhi hundi ya mkopo wenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Mbili na Hamasini kwa vikundi 40 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu. Mkopo huo usio na riba unaotokana na mapato ya asilimia kumi ya Halmashauri. Halmashauri ya Mji wa Korogwe imepanga kutoa Mkopo wa asilimia kumi kwa awamu nne katika mwaka wa fedha 2024 /2025. Mkopo wa awamu ya kwanza umetolewa Desemba 18, Mwaka huu (2024) katika Ukumbi wa Halmshauri ya Mji wa Korogwe. Mgeni rasmi katika utoaji wa mkopo huo alikua Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.