Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Kampuni ya Vodacom imeanza kutoa matibabu bure kwa Wakazi wa Mji wa Korogwe na Maeneo Jirani. Huduma zitatolewa kwa muda wa Siku tatu (3) kuanzia Julai 21 – Julai 23, 2025 katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe (TTC) Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Huduma zinazotolewa katika Kambi hiyo ni pamoja na Uchunguzi na Matibabu ya Macho, Afya ya Kinywa na Meno, Afya ya Akili, Saratani ya mlango wa shingo ya kizazi na matiti, kisukari, pua, masikio, Magonjwa ya Tezi Dume, Homoni , Afya ya Watoto na Homa ya Ini na Wanatarajia kuwahudumia Wagonjwa 342 kwa Siku.
Naye Daktari bingwa wa magonjwa ya Pua, Masikio na Koo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Jimmy Ernest alisema “kuwa baadhi ya Wagonjwa wananchangamoto sio kubwa sana inaweza kutibika kama Wagonjwa watawahi matibabu mapema kwenye Hospitali na Vituo vya Afya. Kwa upande mwingine Mama wa Mtoto Mahili Hemed aliyepatiwa matibabu ya changamoto ya kuota nyama ya pua pamoja na Masikio kutoka kwa Dkt. Jimmy ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Huduma karibu na Wananchi kwani imeturahisishia kupata Huduma karibu hapo zamani tulikuwa tunasafiri umbali mrefu Kwenda kupata Huduma .
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.