Maafisa mifugo kutoka kata 11 za Halmashauri ya Mji wa Korogwe wamefanya zoezi la kuchanja na kuvalisha hereni mifugo katika Mtaa wa Mahenge kata ya Kwamndolwa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Zoezi hili litafanyika maeneo mbalmbali ya Mji wa Korogwe ila kwa leo zoezi la uchanjaji na uvalishwaji wa hereni kwa mifugo ulifanyika kwenye zizi la mfugaji Bw. Mikaelii Samsoni na Bi. Ester Jonathan kwa kuchanja Ng’ombe na Mbuzi. Uchanjaji na uvalishwaji wa hereni ulifanyika Septemba 2, Mwaka huu (2025) katika Mtaa wa Mahenge kata ya Kwamndolwa. Jumla ya Mifugo 320 ilichanjwa na kuvalishwa hereni kati ya mifugo hiyo 205 ni Ng’ombe na Mbuzi 115.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.