Kamati ya Fedha yakagua Miradi ya Maendeleo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala (Madiwani, Mkurugenzi pamoja na Wataalamu wa Halmashauri) amefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa. Ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo ilifanyika ikiwa ni sehemu ya ukamilishaji wa Kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya Pili katika Mwaka wa Fedha 2023 / 2024. Ziara hiyo ilifanyika Februari 8, Mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala walitembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa lengo la kuona ni namna gani Miradi inatekelezwa ili Miradi hiyo iweze kuchagiza ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri pamoja na kuwaletea Wananchi huduma jirani na maeneo yao. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Vibanda vya Biashara katika Soko la Manundu, Uboreshaji wa Vibanda vya Biashara katika Stendi ya Zamani ya Manundu pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Lwengera Darajani iliyoko Kata ya Old Korogwe.
“Nitoe pongezi kwa Mkurugenzi pamoja na Wataalamu wote wa Halmashauri kwa kukamilisha Mradi wa Ujezi wa Vibanda vya Biashara kwa wakati, kukamilika kwa Vibanda hivi kutasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri” Alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati akikagua Mradi wa Ujenzi wa Vibanda vya Biashara katika Soko la Manundu. Mhe. Komba alifafanua kuwa kuongezeka kwa Vibanda vya Biashara katika Soko la Manundu kutaisaidi Halmashauri kuwa na vyanzo vya mapato vyenye uhakika.
“Kadri fedha zitakapopatikana, Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kushirikiana na Madiwani itaendelea na jitihada za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuongeza vyanzo vya mapato katika Halmashauri pamoja na kuwasogezea huduma Wananchi jirani na Maeneo yao”. Alisema Bw. Elinlaa Kivaya ambaye ni Mchumi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati wa Ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo akimwakilisha Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.