Kamati ya uhakiki wa mikopo Wilaya yafanya ziara ya kuhakiki vikundi vinavyostahili kupewa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani na fedha za marejesho ya vikundi kwa Halmashauri ya Mji Korogwe kwa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kamati hiyo imeongozwa na Kaimu Katibu Tawala Bi. Glory Sanga, mwakilishi kutoa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga Bw. Charles Mtali, Afisa TAKUKURU, na mwakilishi wa OCD Korogwe pamoja na ofisi ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Korogwe.
Ziara hiyo imefanyika Novemba 25 na kumalizika Novemba 26, 2025 katika kata mbalimbali zikiwemo Kwamsisi, Mtonga, Kilole, Magunga, Masuguru, Majengo, Old Korogwe, Manundu na Bagamoyo. Vikundi 15 vimebainishwa kuomba mkopo na kufanyiwa tathmini kama walivyoomba. Lengo la ziara hiyo ni kuhakiki miradi ya vikundi.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Korogwe Bi. Glory Sanga ambaye ni mwakilishi wa Katibu Tawala Wilaya Korogwe amewataka wanavikundi kuchukua mkopo na kufanya mradi utakaowawezesha kurejesha.Baada ya ziara hiyo kikao cha tathmini ya uhakiki wa vikundi vinavyotarajiwa kupewa mikopo Wilaya kwa kipidi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026 kilifanyika.
Aidha Mratibu wa mikopo asilimia 10 Bi.Rahma Kahelo kwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya jamii ngazi za Kata ameahidi kufuatilia kwa kina miradi itakayoanzishwa na kila kikundi ili kuhakikisha lengo la utoaji wa mikopo hiyo linatimia kwa kila mwananchi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.