Kampeni ya kupinga Ukatili wa Kijinsia yasonga mbele katika Mji wa Korogwe
Katika harakati za mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe pamoja na Viongozi wa Dini wamendelea na Kamapeni ya kupinga ukatili huo kwa kutembelea Shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Agosti 14, Mwaka huu (2024), Wataalamu wa Mji wa Korogwe, Vongozi wa Dini pamoja na Mratibu wa Mradi wa US Aid Kizazi Hodari walitembelea Shule ya Msingi Silabu iliyopo Kata ya Old Korogwe. Lengo la kutembelea Shule hiyo ni kukutana na Wanafunzi pamoja na Walimu ili kuzungumza nao, kupokea maoni yao pamoja na kuelimishana mbinu za kupinga ukatili wa Kijinsia kwa Wanafunzi katika maeneo ya Shule na Familia kwa ujumla.
“Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia vimeongezeaka ni vyema kuwaelimisha Wanafunzi ili waweze kutoa taarifa kwa Walimu, Wazazi pamoja na Walezi pindi wanapokumbana na ukatiki huo”. Alisema Bi. Happya Luteganya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wakati akizungumza na Walimu wa Shule ya Msingi Silabu. Kwa upande mwengine Bi. Luteganya amewataka Wanafunzi kujiepusha na tabia ya kukaa karibu na Watu wenye tabia mbaya pamoja na kupokea vitu vya bure kwa watu ambao hawana nasaba nao.
Nae Bi. Sponsa Mhagama ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Silabu aliwashukuru Wataalamu wa Mji wa Korogwe, Viongozi wa Dini pamoja na Mratibu wa Mradi wa US Aid Kizazi Hodari kwa kutembelea shuleni hapo. Bi Mhagama alisema “Natoa shukrani zangu za dhati kwa Watu wote mliokuja kututembelea hapa Shuleni, swala la mapambano ya Ukatili wa Kijinsia kwa Watoto sio jukumu la Walimu pekeyeo hili ni jukumu la Jamii nzima”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.