Katibu Tawala Wilaya ya Korogwe atoa msaada Gereza la Korogwe
Kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, Katibu Tawala Wilaya ya Korogwe akiwa pamoja na Kamati ya maandalizi za sherehe za uhuru wa Tanganyiaka Novemba 23, mwaka huu amekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Korogwe lililopo Korogwe Mjini. Msaada huo uliotolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Korogwe unajumlisha Sukari, Mchele, Mafuta ya kupikia, Dawa za meno pamoja na Sabuni.
“Katika kusheherekea miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, Serikali tumemiletea zawadi ili tuweze kufurahi kwa pamoja” alisema Bi. Rahel Mhando ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya korogwe. Bi. Rahel alifafanua kuwa sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, zitakazofikia kilele chake Desemba 9, mwaka huu, inasheherekewa na wananchi wote ikijumlisha waliopo magerezani.
Katika Hatua nyengine, Bi. Rahel amewataka Vijana wanatumikia vifungo Gerezani, baada ya kumaliza vifungo vyao kuwa waadilifu watakaporudi katika jamiii ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwa leo la kuimarisha uchumi wao na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Bi. Rahel alisema “mtakaporudi katika jamii kuweni waadilifu”.
“Tunatoa shukrani kwa Uongozi wa Wilaya ya Korogwe na Serikali kwa ujumla kwa kutupatia msaada” alisema SP. Godfrey Mhando ambaye ni Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Korogwe. SP. Mhando alifafanua kuwa wafungwa sio tu wanahitaji kupewa msaada na Serikali bali Wananchi wote wanakaribishwa kuonana na uongozi wa Magereza iwapo wanahitaji kutoa msaada.
Katika hatua nyingine, Wafungwa waliokabidhiwa msaada wa vifaa mbailmabali walitoa shukrani kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe na Serikali kwa ujumla kwa kuwapatia msaada.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.