Katika kikao kilichofanyika ukumbi wa halmashauri mwishoni mwa wiki iliyopita huku akiwepo mbunge wa Korogwe mji Mhe. Mary Chatanda taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwezi Mach hadi Juni ilisomwa.Kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa 2017/2018 halmashauri ilifanikiwa kukusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi 296,036,700.46 na kutumia 288,148,364.56.Pia halmashauri ilipokea ruzuku jumla ya shilingi 5,369,511,377.35 na kufanya jumla ya ruzuku na makusanyo ya ndani kuwa 5,665,548,077.81.Hata hivyo jumla ya shilingi 1,273,634,431.59 katika miradi ya maendeleo.
Baraza hilo pia limepitia na kuidhinisha taarifa mbalimbali zilizotokana na vikao vya kamati zote zakudumu za halmashauri ikiwepo kamati ya fedha na uchumi,Mipango miji na mazingira,kamati ya elimu ,afya na maji, pamoja na kamati ya kuthibiti ukimwi.Taarifa zote zimeonyesha utekelezaji wa kina wa shughuli za kimaendeleo zilizofanywa na halmashauri kwa kipindi chote cha robo ya nne ya mwaka ulioishia mwezi juni 2018.
Aidha baraza la madiwani pamoja na mbunge wameipongeza timu ya UMISETA iliyofanya vizuri katika mashindano ya shule za sekondari mwaka huu ambapo ilifanikiwa kuwa yakwanza kimkoa na pia kuwezesha mkoa wa Tanga kuwa wa kwanza kitaifa.Kwa ushindi huo Mbunge aliahidi kuwachangia (poketi mane) katika safari yao kwenda mbuga za wanyama ili kukuza sekta ya utalii.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.