Mwenyekiti wa kamati ya lishe Halmashauri ya Mji wa Korogwe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bw. William Mwakilema aongoza kikao cha utekelezaji mkataba wa lishe katika ilani ya chama tawala ngazi ya Halmashauri kwa robo ya kwanza July - Septemba 2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Hospitali Halmashauri ya Mji wa Korogwe Novemba 19, 2025. Bw. Mwakilema amempongeza Afisa Lishe kwa kuongeza asilimia za utoaji lishe na utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe kwa kadi alama (score card) katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kipindi cha Julai- Septemba 2025.
Aidha Bw. Mwakilema amewasisitiza wajumbe wa kikao hicho kushirikisha wananchi katika kuhakikisha usalama na kubaini wageni wasiowatambua katika makazi yao. Pia alisisitiza idara ya Maendeleo ya Jamii kutoa elimu na kuwashauri walengwa wa mikopo kufikriri biashara za kilimo kwani kinaweza ongeza tija zaidi katika ustawi wa maendeleo yao.
Naye Katibu wa kikao hicho Bi. Zahara Msangi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe amewapongeza na kuwahimiza kuongeza jitihada za usimamizi wa utekelezaji wa afua za lishe katika ngazi ya Kata na Vijiji na kuimarisha uanzishaji wa bustani za mboga mboga katika shule za Msingi na Sekondari ili kuwezesha uhakika wa chakula shuleni.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.