Komba: Madiwani ongezeni nguvu katika usimamizi wa Miradi ya Maendeleo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba amewataka Madiwani wa Halmashauri hiyo kuongeza nguvu katika usimamizi wa Miradi ya Maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati kwa lengo la kuwahudumia Wananchi. Kauli hiyo aliitoa Aprili 25, Mwaka huu wakati Kamati ya Fedha na Utawala ilipotembelea Miradi ya Maendeleo katika Maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
“Waheshimiwa Madiwani ongezeni nguvu katika usimamizi wa Miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati” alisema Mhe. Francis Komba wakati wa ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Mji wa Korogwe. Mhe. Komba alifafanua kuwa swala la usimamizi wa Miradi sio jukumu la Mkurugenzi na Wataalamu wa Halmashauri pekeyeo, hivyo ni vyema Madiwani wakaongeza nguvu ili kuharakisha kukamilika kwa miradi hiyo.
Katika hatua nyengine, Mhe. Komba amemshauri Mkurugenzi wa Halmashuri ya Mji wa Korogwe kuendeleza utamaduni wa uwazi katika utoaji Kandarasi za Ujezi pamoja na ushirikishwaji wa Kamati za Ujezi katika Manunuzi ya Vifaa ili kuleta umoja na mshikamano katika usimamizi wa Miradi. Mhe Komba alisema “Tuendeleze utawaduni wa uwazi katika utoaji wa Kandarasi za Ujezi pamoja na Manunuzi ya Vifaa ili kuondoa ukakasi kwa Wananchi”
“Mheshiwa Mwenyekiti, Madiwani tuko tayari katika kuongeza nguvu katika usimamizi wa Miradi ili iweze kukamilika kwa haraka”alisema Mhe. Nassoro Mohamed amabye ni Diwani wa Kata ya Kwamsisi. Mhe. Nassoro alifafanua kuwa Miradi ya Maendeleo inapokamilika kwa wakati ni jambo jema kwa Mkurugenzi pamoja na Madiwani kwa ujumla. Nae Bw. Elinlaa Kivaya ambaye ni Mchumi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe anayemwakilisha Mkurugenzi alisema “Mwenyekiti maelekezo yote uliyotupa tumeyapokea na tutatekeleza”.
Ziara ya Kamati ya Fedha na Utawala inayojumuisha Madiwani pamoja na Wataalamu wa Halmashauri ilitembelea Miradi mbalimbali katika kuhitimisha Robo ya Tatu katika Mwaka wa Fedha 2022/23. Miradi ya Maendeleo iliyotembelewa ni Pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Vibanda vya Biashara katika Uwanja wa Manundu, Ujenzi wa Barabara ya Lami Hojana / Magufuli (Mt.View), pamoja na Ujenzi wa Zahanati ya Old Korogwe ( Lwengera Darajani).
Miradi mingine ni pamoja na Ujenzi wa Zahanati ya Kilole ( Kilole Manzese), Ujenzi wa Mifereji katika Barabara ya Madaraka (Kilole Darajani), Ujenzi wa Bweni la Watoto wenye Mahitaji Maalumu katika Shule ya Msingi Kwamngumi, pamoja na Ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Kibiashara kilichopo Makao Makuu ya Halmashauri.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.