Komba: Wakandarasi kamilisheni miradi kwa wakati
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba amewataka Wakandarasi wanaotekeleza miradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili uweze kufikia lengo lililokusudiwa. Mhe. Komba alitoa kauli hiyo wakati wa Ziara ya Madiwani wa Kamati ya Fedha na Utawala walipofanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa inayotekelezwa na Serikali kupitia mradi wa “BOOST”. Zira hiyo ya kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe ilifanyika Novemba 1, 2024.
“Wakandarasi hakikisheni mnakamilisha miradi kwa wakati ili tuweze kufikia lengo tuliojiwekea” alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mhe. Komba alisisitiza kuwa Serikali haitomvumilia Mkandarasi yoyote ambaye atatekeleza mradi chini ya kiwango au atashindwa kukamilisha mradi kwa wakati.
Ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ni sehemu ya kukamilisha Kikao cha Madiwani katika kipindi cha Robo ya Kwanza katika Mwaka wa Fedha 2024 / 2025. Katika ziara hiyo Mhe Francis Komba aliambatana pamoja na Madiwani, Wataalamu pamoja na Bi. Mwashabani Mrope ambaye ni Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.