Maadhimisho hayo yalifanyika katika uwanja wa manundu hapo jana ambapo huadhishwa duniani kote kila tarehe 8 mwezi wa tisa lakini kwakuwa tarehe hiyo Tanzania kulikuwa na mitihani ya darasa la saba imehamishiwa siku ya jana.Sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bi. Gwakisa Kasongo akiwakilishwa na afisa elimu msingi wa Halmashauri ya mji wa korogwe Ndugu Kassim Kaoneka Athman.Pia zilijumuisha viongozi wote wa elimu wa halmashauri,walimu na wanafunzi wa shule zote za msingi pamoja na RoomToRead waliokuwa waandaaji na waendeshaji wa maadhimisho hayo.Yalihusisha pia wanafunzi wa shule za msingi na walimu wake,ambapo baadhi ya shughuli zilizofanyika ni pamoja na maonesho ya maktaba ya kusomea,mbinu za ufundishaji madarasa ya awali,shindano la kusoma na kusimulia hadithi pamoja na maigizo; vyote vikifanywa na wanafunzi madarasa ya awali.
Shughuli zote zimeandaliwa na RoomToRead ambalo ni shirika lisillo la kiserekali lakini linafanya kazi na Serekali katika baadhi ya shule za msingi kuweka mazingira bora ya wanafunzi kujua kusoma na kuandika.Shirika hili linahusika zaidi na kuwajengea uwezo waalimu wa madarasa ya awali pamoja na kuandaa na kuchapisha vitabu na vijarida vya kujisomea.Pia huziwezesha shule zote za msingi kuwa na maktaba kwa ajili ya kujisomea.Shirika hili ambalo lipo mikoa michache Tanzania, kwa upande wa Tanga lipo tu Korogwe mjini na Handeni.
Siku hii ina umuhimu mkubwa kwa taifa la Tanzania kwani inalenga kuondoa adui ujinga kwa kizazi kijacho.Kwa maana nyingine ni kwamba kila mwanafunzi akimaliza darasa laba atakuwa na uwezo wa kusoma na kuandika na hivyo kumrahisishia kuendelea na masomo ya sekondari bila shida.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.